Rais wa Yanga Eng.Hersi Said amefanya mazungumzo na Waandishi wa Habari kuelezea mambo 7 ambayo mashabiki wa Yanga wanapaswa kuyafahamu.. Nimekuwekea nukuu ya mambo machache kati ya mengi aliyozungumza Eng.Hersi Said
1.Umuhimu wa GSM ndani ya Yanga
“Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea dua liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno.
“Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu fulani, alikuja na kutuuliza bajeti ya Bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda,”
“Kila unapoona Wanayanga wanakunywa supu, ujue ni maadhimisho ya zile goli 5. Nimemwambia Ally Kamwe zoezi hili liendelee kwa sababu linatukumbusha tukio lililotupa raha sana mashabiki wa Yanga”
2.Usajili wa Chama
“Chama ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa sana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ana ambao 19 mpaka sasa, kwa ubora wake kwa Msimu huu hakuna timu aliyostahili kucheza Afrika zaidi ya Yanga.
“Nilizungumza nae na kumwambia anakuja kwenye timu ambayo imesheheni ubora kila eneo, itamsaidia kufikia mafanikio makubwa zaidi. Chama aliichagua Yanga kwa sababu ya ubora wa kikosi chetu.
3.Hatma ya Gamondi
“Kabla ya kusaini mkataba mpya, Kocha wetu Miguel Gamondi alipata ofa nyingi sana kutoka Klabu nyingine kubwa Afrika na aliahidiwa hela nyingi lakini alichagua kubaki Yanga kwa sababu ya ubora wa timu tuliyoitengeneza. Hii timu yetu inaweza kumpa heshima kubwa zaidi Afrika,”
4.Tageti ya michuano ya kimataifa
“Malengo yetu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni tufike tena Hatua ya Robo Fainali. Lakini kwenye maisha M/Mungu hutoa zawadi, tukipata zawadi ya kufika Fainali na kuchukua Ubingwa basi tutashukuru. Target yetu ni Robo Fainali na tutapambana kufanikisha hilo,”
5. Udhamini klabuni
“Tumekuwa na mahusiano mazuri ya wadhamini wetu ambao kila tunapowakimbilia wanatushika mkono, nichukue fursa hii kuwashukuru sana Kampuni ya SportPesa, Azam TV na GSM kwa kuwa na sisi katika kipindi chote cha Uongozi wangu”
6.Sakata la Mzize
“Kila mchezaji anayecheza Yanga anatakiwa na timu nyingine Afrika. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu tuna wachezaji bora sana katika kikosi chetu.
“Walid Mzize ni tegemeo la taifa letu. Makocha wote wawili wa Yanga [Nabi na Gamondi] wamempa nafasi. Kwa sasa yuko kwenye mikono salama zaidi akiwa na jezi ya Yanga na ana mengi ya kujifunza na hapa ndio mahala sahihi kwake kwa maslani ya timu yetu ya Taifa pia”
7. Mchezo wa marudiano na Vital’o
“Kutokana na marekebisho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa, mechi yetu ya marudiano dhidi ya Vital’O, hatutacheza tena uwanja wa Mkapa, Tutacheza katika uwanja wa Azam Complex, Jumamosi majira ya saa 1:00 jioni.
“Mechi iliyopita wenzetu Vital O walisema watatunywa kama supu lakini tulifanikiwa kupata ushindi wa Goli 4, Lakini kwenye mchezo huu wa marudiano ni zamu yetu sasa kuwanywa wao kama supu.”