Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga amesema waliandaa usiku maalum wa SIKU YA UTALII kama sehemu ya Tamasha la Kizimkazi 2024, ili kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vilivyopo Zanzibar.

Soraga ameyasema hayo wakati akizungumza na mamia ya wadau na washiriki waliohudhuria tukio la USIKU WA UTALII katika Tamasha la Kizimkazi 2024 lililofanyika kwenye uwanja wa Maendeleo ya Sheria wa Dimbani, Kizimkazi, Zanzibar.

Amesema, “tumeona ni vema tutumie fursa hii kutangaza vivutio vyetu kwani tunaamini tukitumia fursa hii, wageni wengi watakuja Zanzibar.”

Aidha Soraga pia ametumia fursa hiyo kuwaomba watalii na wawekezaji wanaokwenda Zanzibar wazingatie suala la kuhifadhi na kutunza mazingira.

Naye, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma alisisitiza haja ya kuendelea kutumia utamaduni kama moja ya vichocheo vya utalii. “Tunapofanya matamasha haya ni lazima tulinde mila na desturi zetu,” alisema.

Ahmed Ally afunguka kinachowanyima furaha wanasimba
Majaliwa: Zikitumika vizuri zitaongeza idadi ya Watalii