Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume ya Kimahakama ya majaji, ili kuchunguza madai ya watu waliotekwa na kupotea nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya utekaji nchini akidai mpaka sasa zaidi ya watu 80 wametekwa na Jeshi la Polisi lipo kimya.
“Tumeamua tupaze sauti kuwataka wenye mamlaka nchini kutambua kwamba thamani ya maisha ya kila Mtanzania mwenzetu ni kubwa kuliko kitu chochote, kwa hiyo sisi kama Jamii ya Tanzania ni wajibu wetu kisimama kuhakikisha haki kwa watu wote inapatikana na tusiendelee kuruhusu baadhi ya vyombo vya dola kuwatesa na kuwapoteza Watanzania na sisi tukakaa kimya,” amesema Mbowe.
Aidha, amemuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika kumwandikia wakala maalumu Rais Samia juu ya Suala hilo, ili kuweza kupata suluhu ya usalama wa uhuru wamaisha ya watu ambao sasa upo shakani.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 23, 2024
Othman: Hoja za ACT zimewaelemea