Bado nawajuza kuhusu maajabu ya Ulimwengu safari hii nikikupa kisa cha mwaka 2018 ambapo kijana mmoja billionea na mrithi pekee wa kampuni moja ya kibiashara ya nchini Uhispania, yeye alitoweka ghafla nyumbani kwao na jitihada za kumtafuta zikagonga mwamba.
Baada ya miaka sita mmoja wa Wafanyakazi wake alishangaa kumkuta tajiri yake akiwa kijiji kimoja huko Bolivia akifanya za vibarua katika shamba la Tufaa wenyewe mnaita Apple.
Alimuhoji kwa mshangao na alijibiwa kuwa aliamua kutoroka nyumbani ili aishi maisha ya kawaida kama binadamu wengine duniani wanavyoishi na kuachana na maisha ya anasa za kibilionea aliyokuwa akiyaishi tangu utoto wake.
Hata hivyo familia yake ilifurahi kupata habari za ndugu yao na wakaamua kumuacha aendelee kuishi na maisha aliyoyachagua.
Kilichofuata ni Wakulima wengi amba walikuwa wakimpa kazi za vibarua wakaanza kumheshimu na kuona aibu ya kumpa tena vibarua kama ilivyokuwa mwanzo.
Kisa hiki ni hadithi ya kusisimua tu lakini kiuhalisia hii style haiwezekani, yaani haiwezi ikatokea, narudia tena haiwezekani.