Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es salaam – DAWASA, wameliomba Baraza la Madiwani la mji wa Kibaha heka kumi za ardhi kwaajili ya kuchakata taka tope (maji taka) kutoka majumbani katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

Akitambulisha mradi huo Mhandisi wa DAWASA kutoka Dar es salaam Injinia Hamad Msemo katika Baraza la Madiwani la mji wa Kibaha mkoani Pwani amesema mradi huo utagharimu shilingi Bililoni 2.7 na fedha hizo tayari zimepatikana ambapo kwasasa zinasubiri maamuzi ya Baraza hilo la Madiwani.

Amesema fedha hizo shilingi Bililoni 2.7 ni ufadhiri kutoka Banki ya Dunia zitajenga aina mpya ya mifumo ya kuchakata taka tope kutoka majumbani katika mikoa hiyo ya Dar es salaam na Pwani.

Alisema miundombinu hiyo mipya itafunika taka tope hilo ardhini ambapo maji wala tope hilo kutoka majumbani halitaonekana wazi na kusababisha kero kwa wananchi labda kwa sababu maalumu itakayohitajika.

Injijia Hamad alisema mifumo kama hiyo tayari ujenzi unaendelea pia jijini Dar es salaam katika maeneo ya Kigamboni, Ilala, Temeke na Ubungo ambapo Halmshauri itanufaika kwa kupata fedha kutoka kwa kila gari litakalofika kumwaga taka tope katika eneo hilo kutoka majumbani.

“Kwasasa kuna miradi nane inayotekelezwa kwa kujengwa katika Jiji la Dar es salaam na Pwani ambapo kati yake ipo miradi mikubwa miwili ambayo inaweza kuchakata Lita laki moja na sabini kwa siku ambayo kati yake miwili inatekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni na mwingine tunaomba tupewe eneo hapa Kibaha”

“Hii miradi ni ya kisasa zaidi ni baada ya mitambo wa vingunguti na kurasini kuepuka harufu na kero zingine tukaona tuje na mfumo wa kisasa zaidi ambapo uchakataji wake utafanyika pia kwa kupanda vitaru vya kiti”

Alisema “Mfumo huo utakuwa na mgawanyiko wa sehemu saba ikiwemo sehemu ya kudampo hizo taka tope ambapo magari ya taka yatakuwa yakimwaga taka tope ambayo sehemu hiyo itatumika kuchuja hilo taka tope”

“Baada ya hapo taka tope hilo litaingia kwenye hatua ya kutibiwa kwa uchafu kushuka chini na maji kuendelea katika hatua inayofuata ya maji kutulia ili uchafu ushuke chini na maji ya kijaa katika ujazo mkubwa maji yatahamia katika hatua ya tatu ya kupita katika vyumba vingine vidogo vidogo ikiwa ni pamoja na kuingizwa katika chumba chenye kokoto ndogo ndogo ambazo hutumika kama chujio” alisema Eng. Hamad.

Aidha Mwenyekiti wa Halmshauri ya mji wa Kibaha Musa Ndomba amesema Madiwani wanahitaji elimu zaidi hasa kwa kumtembelea kwenye maeneo yaliyowekwa ili wakajifunze zaidi.

Serikali yarejesha huduma za kijamii Ngorongoro
Mgomo: Biashara za nje zafunga soko kuu Morogoro