Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI), umeungana na Watanzania, watetezi wa haki za binadamu hasa ule wa haki za Wanawake na Wasichana kukemea ukatili wa kijinsia aliofanyiwa binti mmoja mkazi wa Yombo, jijini Dar es Salaam.

Kupitia maazimio yaliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Transforming Life, Nashivai Mollel ametaka Jeshi la Polisi liwajibike kwa kumchukulia hatua Afande anayetajwa aliyehusika kuwatuma Vijana watano kutekeleza ukatili huo.

Aidha, amesema makosa yaliyotajwa ni machache licha ya ushahidi wa video unaoonesha yapo mengi zaidi, ikiwemo ubakaji wa kundi, usafirishaji wa mtoto kingono, ulawiti, kula njama za kutekeleza uhalifu, kuteka nyara na shambulio la kudhuru.

Wamelitaka Jeshi la Polisi piq kumkamata mtuhumiwa mwingine ambaye anadaiwa kuwa chanzo cha ukatili huo kwa kuwa na mahusiano na binti huyo, mwanaume ambaye anadaiwa kuwa hawara wa afande.

Wamesema myu huyo anatakiwa awajibike kwa kufunguliwa mashitaka ya usafirishaji wa kingono chini ya kifungu cha 6 (1) 6 (4) cha sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu sheria namba 6/2008 ikisomwa pamoja na sheria ya nyongeza namba 2/2022.

Kambi ya masomo: Shule tano zakabidhiwa Chakula Msoga
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 23, 2024