Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema hatashiriki kukandamiza haki ya mtu mahala popote pale atakapokuwa na akikumbusha kuwa nafasi wanazopata Viongozi ni upendeleo wa Mungu.

Makonda ameyasema hayo hii leo Agosti 23, 2024 wakati akizungumza na Wananchi wa kata 11 zilizopo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha katika eneo la Oloirobi, lililopo Kata ya Ngorongoro.

Amesema, “mimi mtoto wenu na mtumishi wenu lakini nina sifa nyingi mojawapo ni sifa ya kusimamia haki na ukweli, hiyo nilikula kiapo kwamba popote nitakapokuwepo kwenye nafasi yoyote sitashiriki kukandamiza haki ya mtu na sikuishia hapo nikasema nafasi hizi tunazopata ni za upendeleo wa Mungu.

Ameongeza kuwa, “lakini Mungu anapotupa nafasi anataka tufanye kazi kwa watu wake aliowaumba kwa mfano wake, furaha niliyonayo chama changu cha mapinduzi (Chama Cha Mapinduzi-CCM) ambacho mimi nilikitumikia kama mwenezi.”

Akiwa katika eneo hilo, Makonda aliambatana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, William Lukuvi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 24, 2024
Picha: Amiri Jeshi Mkuu katika Maadhimisho Miaka 60 ya JWTZ