Sote tunafahamu kwamba Uongozi ni mamlaka au karama ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo na kipimo chake huwa ni jinsi gani Kiongozi huyo anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.

Kimantiki Kongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu walio chini yake. Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.

Sasa leo tunaangalia 10 bora ya Viongozi mahiri wa wakati wote barani Afrika, ambao wakati wa uongozi wao na hata leo bado wameacha alama isiyofutika itakayodumu vizazi na vizazi kutokana na utendaji wao.

1. Thomas sankara πŸ‡§πŸ‡«

Thomas Isidore NoΓ«l Sankara ( Desemba 21, 1949 – Oktoba 15, 1987) huyu alikuwa ni Afisa wa Kijeshi wa Burkinabe (Burkina Faso), ambaye ni mwanamapinduzi wa Kimarxist na Pan-Africanist aliyewahi kuwa Rais wa taifa hilo toka mwaka 1983 hadi kuuawa kwake mwaka 1987.

2. Muammar Gaddafi πŸ‡±πŸ‡Ύ

Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi ( Juni 7, 1942 – Oktoba 20, 2011), alikuwa Mwanamapinduzi, Mwanasiasa na Mwananadharia wa kisiasa wa Libya aliyetawala Libya kuanzia 1969, hadi kuuawa kwake na waasi mwaka 2011.

 

3. Patrice Lumumba πŸ‡¨πŸ‡©


Patrice Γ‰mery Lumumba (Julai 2, 1925 – Januari 17, 1961), alikuwa ni Mwanasiasa na Kiongozi wa uhuru wa Kongo (Zaire), ambaye aliwahi pia kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong kuanzia Juni hadi Septemba 1960, alikuwa ni Mwanaharakati wa Kitaifa wa Kongo (MNC) kuanzia mwaka 1958 hadi kunyongwa kwake Januari 1961.

4. Jomo Kenyatta πŸ‡°πŸ‡ͺ

Jomo Kenyatta ( alifariki Agosti 22, 1978), alikuwa ni Mwanaharakati wa kupinga ukoloni wa Kenya na Mwanasiasa ambaye alitawala Kenya kama Waziri Mkuu toka 1963 hadi 1964 na kisha kama Rais wa kwanza wa Taifa hilo kutoka 1964 hadi kifo chake mwaka 1978.

5. Nelson Mandela πŸ‡ΏπŸ‡¦

Nelson Rolihlahla Mandela (Julai 18, 1918 – Desemba 5, 2013), alikuwa niΒ  Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuanzia 1994 hadi 1999.

6. Robert Mugabe πŸ‡ΏπŸ‡Ό

Robert Gabriel Mugabe (21 Februari 1924 – 6 Septemba 2019), alikuwa ni Mwanamapinduzi wa Zimbabwe na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe kuanzia 1980 hadi 1987 na kisha Rais kuanzia 1987 hadi 2017.

7. Julius Nyarere πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere (13 Aprili 1922 – 14 Oktoba 1999), alikuwa Mwanaharakati wa kupinga ukoloni wa Kitanzania, Mwanasiasa na Mwananadharia wa kisiasa.

Alitawala Tanganyika kama Waziri Mkuu kuanzia 1961 hadi 1962 na kisha kama Rais wa Tanganyika kuanzia 1962 hadi 1964, na kisha akaongoza Tanzania, kama rais kuanzia 1964 hadi 1985.

8. Kwame Nkrumah πŸ‡¬πŸ‡­

Francis Kwame Nkrumah (21 Septemba 1909 – 27 Aprili 1972), alikuwa Mwanasiasa wa Ghana, Mwananadharia wa kisiasa, na Mwanamapinduzi.

Alihudumu kama Waziri Mkuu wa Gold Coast kuanzia 1952 hadi 1957 ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza na kisha Rais wa Ghana, kutoka 1957 hadi 1966.

9. Haile Selassie πŸ‡ͺπŸ‡Ή

Haile Selassie (23 Julai 1892 – 27 Agosti 1975), alikuwa Mfalme wa Ethiopia kutoka 1930 hadi 1974. Alipanda mamlaka kama Regent Plenipotentiary wa Ethiopia (Enderase) kwa Empress Zewditu kutoka 1916 hadi 1930.

10. Kenneth Kaunda πŸ‡ΏπŸ‡²

Kenneth Kaunda (28 Aprili 1924 – 17 Juni 2021), pia anajulikana kama KK, alikuwa Mwanasiasa wa Zambia ambaye aliwahi kuwa rais wa kwanza wa Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi 1991.

Nitasimamia shabaha ya kuwa na JWTZ madhubuti - Rais Samia
Vijiji 25 kufanya uchaguzi Serikali za Mitaa Ngorongoro