Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi – INEC, imeviasa vyama vya siasa kutoingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika vituo vya kuandikishia wapiga kura.
Wito huo umetolewa hii leo Agosti 25, 2024 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Mara.
Amesema mawakala au viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji vituoni kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi.
Amehimiza viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya tume, na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
zaidha, amevitaka vyama vya siasa kutumia sheria zilizopo kuwasilisha changamoto zinazojitokeza kwa tume, ambapo ameongeza kuwa INEC itazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi, na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi la uboreshaji. @tumeyauchaguzi_tanzania