Ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’o umeifanya klabu hiyo kujiandikia historia ya kipekee kwa msimu huu baada ya kushinda mabao 4-0 mchezo wa kwanza na kuifanya klabu hiyo kufunga jumla ya mabao 10-0 kwenye michezo miwili kuelekea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Africa.
Rekodi ya awali iliyowekwa na Yanga ni ushindi wa jumla ya mabao 9-1 dhidi ya Zalan FC katika hatua za awali za kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa Africa
kuzaliwa upya kwa Chama
Clatous Chama aliweka rekodi ya kipekee kwa kuhusika na mabao matano Kati ya 6 yaliyofungwa na Yanga. Nyota huyo aliyesajiliwa msimu huu alikuwa mwiba mkali kwa Vital’o baada ya kutengeneza mabao 4 na kufunga bao 1.
Aziz Ki, Clement Mzize,Prince Dube na Mudathir Yahya wote walinufaika na pasi za mwisho za mwamba wa Lusaka.
mtazamo wa kocha
Kocha Miguel Gamondi ameendelea kuimarisha kikosi chake kwa kutumia wachezaji wote waliopo kikosini. mchezo wa pili dhidi ya Vital’o aliwapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika kwenye mchezo wa awali. Jonas Mkude,Abubakar Salum Sureboy, Aziz Andambwile,Musonda,Nickson Kibabage,Duke Abuya na Dickson Job
Wachezaji hawa walionyesha thamani ya uwepo wao uwanjani na kufanya kocha huyo kuwa na kikosi kipana. Ubora wa kila mchezaji utampa nafasi Gamondi kufanya maamuzi ya kuwatumia nyota mbalimbali kulingana na mechi na hatokuwa na wasiwasi kama moja ya mchezaji wake atakumbwa na kadhia ya majeraha.
Mwendelezo wa Michuano
Yanga watavaana na Central Bank of Ethiopia (CBE) kwenye hatua ya pili ya michuano ya ligi ya mabingwa Africa.Mchezo wa Kwanza utapigwa nchini Ethiopia na mchezo wa marudiano utapigwa visiwani Zanzibar.kama Yanga watashinda michezo hiyo basi watafuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.