Takribani Watu 20 wameaga dunia na wengine zaidi ya milioni 5.2 wameathiriwa na mafuriko yaliyosababisha na mvua kubwa na mito iliyojaa maji kupita kiasi kupasua kingo nchini Bangladesh.

Mafuriko hayo yamesababisha janga la kibinadamu kwa raia nchini hiyo kuhitaji kwa dharura chakula, maji safi, dawa na nguo hasa katika maeneo ya mbali ambako barabara zilizofungwa zimekwamisha juhudi za uokoaji na misaada.

Mshauri Mkuu wa Serikali chini ya uongozi wa Mohammad Yunus amesema tayari wamechukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha hali ya kawaida inarejea

Taarifa ya Mshauri Mkuu wa Serikali chini ya uongozi wa Mohammad Yunus imesema tayari wamechukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha hali ya kawaida inarejea.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa zaidi ya Watu 400,000 wamehifadhiwa katika vituo 3,500 vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa mafuriko katika Wilaya 11 zilizoathirika.

Tetesi za Usajili Duniani Agosti 26
Gamondi hana wasiwasi na kikosi chake