Klabu ya Simba Queens imepoteza mchezo wa nusu fainali ya CECAFA dhidi ya Kenya Police Bullets. Simba Queens wamepoteza mchezo huo kwa kufungwa  mabao 3-2,Mabao mawili ya Simba Queens  yakifungwa na Corazone. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ishindwe kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mfumo wa mashindano

Mashindano ya CAF WOMENS CHAMPION LEAGUE  yanahusisha timu kutoka kanda mbalimbali za Afrika. Simba Queens ilifanikiwa kuingia hatua ya makundi kwa kanda ya CECAFA baada ya kuibuka mabingwa wa ligi ya wanawake Tanzania msimu wa 2023/24. Ukanda wa CECAFA unaundwa na timu Bingwa kutoka nchi 8 na kugawanywa makundi mawili. Kundi A liliundwa na CBE women ya Ethiopia, Kenya Police Bullets,Yei Joint Stars FC na Rayon Sports Women fc ya Rwanda.

Kundi B liliundwa na Simba Queens kutoka Tanzania,Kawempe Muslim,PVP Buyenzi na FAD dJibout fc . Simba Queens iliibuka kidedea kwa kushinda mechi mbili na sare moja na ikijikusanyia alama saba na ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali dhidi  ya Kenya Police Bullet. Kama Simba Queens ingeibuka na ushindi kwenye mchezo huo basi ingechgeza fainali dhidi ya CBE au Kawempe na kama ingeshinda mchezo huo basi ingefuzu moja kwa moja michuano ya LIGI YA MABINGWA AFRIKA kwa upande wa wanawake.

 

Ekari 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro
Wafukua miili mitatu ya waliopotea, saba mbaroni