Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uingereza Mswidishi Sven Goran Eriksson amefariki Dunia. Ni wiki chache zimepita tangu  kocha huyo ajitokeze hadharani kuwaaga wanafamilia wa mpira wa miguu kwamba mwisho wa uhai wake umefika.Sven amefariki dunia akiwa na miaka 76 akisumbuliwa na Kansa isiyotibika iliyosambaa mwili mzima.

Sven Goran Erikson ni nani?

Sven Erikson alizaliwa february 5 mwaka 1948 nchini Swideni.Akiwa na miaka 16  alijiunga na klabu ya daraja la nne la Torsby IF akicheza michezo 109 na kufunga mabao 23 kutoka mwaka 1964 hadi mwaka 1971. Mwaka 1972 alijiunga na KB Karlskoga FF akicheza mechi 19 na kufunga mabao 4 . Akiwa beki wa kulia Sven amecheza jumla ya mechi 150 na kufunga mabao 28.

Nafasi yake ya Ukocha 

Sven ni moja ya makocha waliofundisha timu mbalimbali duniani.Kocha huyo amefanikiwa kutwaa makombe 18 ya ligi mbalimbali na  amewahi kuiongoza timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya kombe la dunia mara mbili mfululizo akifanya hivyo mwaka 2002 na mwaka 2006. Kwa Upande wa vilabu Sven amewahi kuvifundisha vilabu vya Manchester City,Benfica,Roma. Hii hapa orodha ya timu alizowahi kufundisha kocha huyo mpaka umauti unamkuta.

1977–1978 Degerfors IF
1979–1982 IFK Göteborg
1982–1984 Benfica
1984–1987 Roma
1987–1989 Fiorentina
1989–1992 Benfica
1992–1997 Sampdoria
1997–2001 Lazio
2001–2006 England
2007–2008 Manchester City
2008–2009 Mexico
2010 Ivory Coast
2010–2011 Leicester City
2013–2014 Guangzhou R&F
2014–2016 Shanghai SIPG
2016–2017 Shenzhen
2018–2019 Philippines

 

Nini kimemuondolea uhai wake 

Sven amefariki kwa saratani ya Kongosho. Mwezi januari mwaka 2024 kocha huyo alitoka hadharani na kutangaza kwamba amebakiwa na miezi michache ya kuishi kutokana na kansa inayomsumbua . Wadau wa soka walihuzunishwa na taarifa hiyo na walimwomba aiongoze klabu ya Wakongwe wa Liverpool kwa mechi moja ya hisani dhidi ya Ajax.

Serikali yapokea gawio la Bilioni 4.35 za TAZAMA
Ekari 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro