Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakary Bin Zubeiry ametangaza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kimataifa ya Qur-an kwa wasichana yatakayofanyika Agosti 31 ,20204 katika Uwanja wa Taifa Benjamin Mkapa.
Mufti Bin Zubeiry amesema hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Dkt. Samia kuhudhuria mashindano hayo ambayo ni ya Kimataifa yatakaowaleta Hifz li Qur-an (Wasomaji Qur-an )kutoka nchi 12 Duniani ambapo pia wajukuu wa magwiji nao watashiriki, ili kupata tuzo maalumu.