Sina shaka sote tumewahi kumuona au kumsikia kiumbe anayeitwa Sokwe, lakini henda kuna jambo hatulifahamu juu yake kuhusu uwezo alionao, Ipo hivi, Mnyama huyu ambaye hupatikana milimani na kwenye mapori makubwa huwa ana nguvu kuliko watu 20.

Sokwe wa milimani wanaweza kuinua au kutupa kitu chochote chenye uzani wa kilo 815. Lakini kuumwa kwake na simba au mamba kunaweza tu kufunika pauni 650 kwa kila inchi ya mraba, wakati kuuma kwake kutafunika pauni 1,300 kwa inchi moja ya mraba.

Mathieu Shamavu, mgambo na mlezi wa Kituo cha Senkwekwe cha Sokwe wa Mlimani, akiwa katika picha ya pamoja na sokwe jike yatima Ndakasi (kushoto) na Ndeze (katikati), katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga iliyopo mashariki mwa Kongo mwaka 2019. Sokwe wa milimani Ndakasi mwenye umri wa miaka 14, alijipatia umaarufu kwa kupiga selfie na muhudumu huyo na alifariki Septemba 26, 2021 baada ya kuugua kwa muda mrefu. (Picha ya Mathieu Shamavu/Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga)

Mpigo wa Sokwe wa milimani unaweza kuponda fuvu la kichwa cha mamba. Lakini Sokwe hawa wa milimani wanatufundisha kwamba ‘nguvu hazifai kutumika kwa ukandamizaji’ kwani licha ya nguvu zao kubwa walizonazo ni vigumu sana kuwakuta wakizitumia vibaya kwa Wanyama wengine.

Badala ya kufanya uharibifu, wao hutumia karibu siku nzima kula na kupumzika.

CDC: Kuna ongezeko kubwa maambukizi homa ya nyani
Barcelona haikamatiki La Liga