Serikali Nchini inaendelea kuchukua hatua katika kusimamia ushindani wa haki na kuwalinda watumiaji wa bidhaa na huduma hapa nchini kwa kutumia Sheria ya Ushindani Na.8 ya Mwaka 2003 inayotarajiwa kufanyiwa marekebisho, ili kuongeza tija.
Kauli hiyo, imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini, Dkt.Oscar Ishengoma Kikoyo ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itatenganisha dhana ya ushindani na dhana ya kuwalinda watumiaji wa bidhaa na huduma nchini.
Akijibu swali hilo, Dkt. Jafo amesema dhana ya ushindani na kumlinda mlaji zina uhusiano mkubwa kwasababu ushindani wenye afya katika soko ni mojawapo ya njia bora ya kumlinda mlaji.
Ameongeza kuwa, kupitia ushindani mteja ananufaika kwa kupata unafuu wa bei, kuongezeka kwa wigo wa kupata bidhaa bora na chaguo sahihi la mlaji, kukuza ubunifu wa wazalishaji wa bidhaa na kudhibiti ukiritimba katika soko.

Daftari la Wapiga kura: Muwepo Vituoni muda wote - Jaji Mwambegele
Picha: Rais Samia katika ufunguzi wa Kikao kazi AICC