Klabu za RB Salzberg,Young Boys na Sparta Prague zimefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa 2024/25. UEFA imetangaza mabadiliko ya kiuendeshaji kwa michuano hiyo kwa kuongeza Timu 4 . Awali michuano hiyo ilikuwa na jumla ya timu 32 na sasa zitakuwa timu 36 likiwa ni ongezeko la timu 4. Baadhi ya vilabu vikongwe kama  Manchester United,Galatasary na Chelsea vilishindwa kufuzu kucheza michuano hiyo.

Vilabu vya Young Boys na RB Salzburg vimekuwa gumzo kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi. Klabu ya RB Salsburg imefanikiwa kuingia hatua za makundi kwa mara ya sita  mfululizo. Young Boys walifanikiwa kufika hatua za makundi baada ya kuwaondosha Galatasary katika hatua ya mtoano wakishinda michezo yote miwili kwa jumla ya mabao 2-0.

Mashabiki wa Manchester United wanaikumbuka vyema Young Boys msimu wa 2021 baada ya timu hizo kukutana hatua za makundi na  Manchester United kulazimishwa sare ya bao 1-1 mchezo wa ugenini na mchezo wa pili uliopigwa Old Traford United walipoteza kwa mabao 2-1. Young Boys walivuna alama 4 kutoka kwa United kati ya alama 5 walizovuna kundi F.

Sparta Prague iliwaondosha wababe wa Swideni Malmo kwa jumla ya mabao 4-0. Mchezo wa kwanza Sparta Prague waliibuka na ushindi wa mabao  2-0 nyumbani  Jamhuri ya Czech  na mchezo wa pili waliibuka na ushindi wa mabao 2-0  ugenini jijini Malmo Sweden.Penati aliyokosa Anders Christiansen kipindi cha kwanza ilipoteza matumaini kwa Malmo na magoli mawili ya  Lukas Haraslin na Albion Rrahmani yaliwaondoa mchezoni Malmo.

Vilabu vya Manchester City,Liverpool,Arsenal na  Aston Villa vitaiwakilisha Uingereza kwenye michuano hiyo na Hispania itawakilishwa na Barcelona ,Girona ,Real Madrid na Atletico Madrid, Italia itawakilishwa na Inter Milan,Ac Milan ,Juventus na Atalanta. Kwa upande wa Ujerumani wao watawakilishwa na Bayern Leverkusen,Bayern Munich na Borrusia Dortmund.

McKay: Kama ni lazima tufe, basi tufe kwa heshima
Dkt. Norman: Mpango wa Afya, lishe shuleni kuimarisha ufaulu