Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndugulile ameshinda uchaguzi wa kiti cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika.

Uchaguzi huo ulifanyika jijini Brazzaville huko Congo, ambapo wajumbe 25 kati ya 46 wa Mkutano Mkuu wa 74 wa WHO walimchagua Ndugulile na kuwashinda wagombea wengine kutoka Niger na Senegal.

Ndugulile ameweka wazi vipaumbele vyake ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya, kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko.

Vipaumbele vingine ni kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.

Kisima cha Maji kuimarisha mahudhurio ya Wanafunzi Mazimbu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 28, 2024