Cristiano Ronaldo ameanza vyema kukiwinda kiatu cha dhahabu kwa mara ya pili mfululizo ndani ya Saudi Arabia. Ronaldo aliiongoza Al Nassr kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Feiha. Mabao ya Al Nassr yaliwekwa kimiani na Talisca aliyefunga mabao mawili dakika ya 5 na 90+5 ,Cristiano alifunga bao moja dakika ya  45 na Brozovic dakika ya 85.

Matokeo hayo yanawafanya Al Nassr kufikisha alama 4 kwenye michezo miwili waliyocheza wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Cristiano Ronaldo na Talisca wanaongoza orodha ya wafungaji bora wote wakiwa na mabao 2 kwenye michezo miwili waliyocheza.

Hatma ya Ronaldo  

Cristiano Ronaldo amesema ataendelea kuwepo nchini Saudi Arabia kwa miaka mingine miwili hadi mitatu na amenukuliwa akisema atastaafu soka akiwa Al Nassr. Nyota huyo mwenye miaka 39 amekuwa na kiwango kizuri tangu alipojiunga na Al Nassr mwaka 2023 akicheza michezo 49 na kufunga mabao 51 pamoja na kutengeneza  mabao 14. Ronaldo hana mipango ya kuwa kocha kwa siku za hivi karibuni na amejipanga kuwekeza nguvu zote kwenye miradi mingine ikiwemo hotel zake za CR7 Pestana , Maji ya kunywa , Utengenezaji wa maudhui kupitia mitandao yake ya kijamii na biashara ya nguo.

 

AICC: Rais Samia afungua kikao kazi Wenyeviti, Wakuu Taasisi za umma
1,000 washindananishwa matumizi Nishati safi ya kupikia