Kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2032 zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia nchini imeendelea kushika kasi baada ya kuandaliwa kwa shindano la kupika lililowashirikisha Mamalishe 1,000 Mkoani Mbeya.

Taasisi za kiserikali na binafsi nchini zimeendelea kujenga ushirikiano wa kikazi, ili kuhakikisha azma hiyo inafikiwa kupitia utoaji wa elimu na uwezeshaji kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini kupitia njia shirikishi za ufikishaji elimu hiyo kama ambavyo Umoja wa Mataifa ukihimiza nchi wanachama kutekeleza lengo namba saba la maendeleo ya milenia linalohusiana na upatikanaji wa nishati safi na nafuu.

Ushirikiano huo, umeshuhudia zaidi ya Mama Lishe 1,000 wa mkoa wa Mbeya wakiingia kwenye mashindano ya upishi yanayoendeshwa na taasisi ya Tulia Foundation kwa kushirikiana na Oryx Gas Tanzania ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa nishati safi ya kupikia.

Mashindano hayo yanalenga kuwahamasisha wajasiriamali wa chakula kutumia nishati mbadala katika kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan sambamba na kudhibiti uharibifu wa mazingira kupitia ukataji miti na matumizi ya kuni na mkaa ambazo zimethibitika kusababisha magonjwa kwa binadamu kwenye mfumo wa upumuaji na kuchangia kwenye ongezeko la vifo.

Meneja miradi ya nishati safi wa Oryx Gas Tanzania, Peter Ndomba amesema mashindano hayo yana tija kubwa kwa wajasirimali hao kwani elimu wanayoipata ikiwemo utunzaji mazingira na wepesi wa upishi wao itayafikia makundi mengi ikiwemo kundi la wateja wa chakula hicho hivyo kuongeza hamasa ya kufikia lengo la Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi na malengo ya Milenia.

Nani kuondoka na kiatu cha ufungaji bora Saudi Arabia?
McKay: Kama ni lazima tufe, basi tufe kwa heshima