Kocha Yusuf Dabo ameendelea kukalia kuti kavu baada ya Azam FC kushindwa kupata ushindi dhidi ya JKT TANZANIA mchezo wa kwanza wa ligi kuu NBC.

Mbali na kuwa na kikosi Chenye wachezaji bora Kocha Yusuf Dabo ameshindwa kuipa Azam FC matokeo chanya kwa msimu huu baada ya kukosa Kombe la ngao ya jamii kwa kufungwa mabao 4 -1 kisha kutolewa michuano ya ligi ya mabingwa Africa na APR kwa wastani wa mabao 2-1.Azam imefanikiwa kufunga mabao 7 na kufungwa mabao 8  kwenye mechi 4 walizocheza hivi karibuni.

Sare ya bila kufungana dhidi  JKT TANZANIA mchezo uliopigwa uwanja wa Meja Isamuyo inamweka kocha huyo katika mazingira magumu kuendelea kutumikia mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu aliobakiza.  Mpaka sasa uongozi wa klabu ya Azam haujasema chochote kuhusiana na hatma ya kocha huyo.

Tetesi za Usajili Duniani 29 agosti 2024
Amtimshia Kobe mwajiri wake ili alipwe mshahara