Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika ya Umma kuendelea kusimamia mageuzi yanayofanywa na Serikali, yanayolenga kuongeza tija kwa wananchi na kuwezesha Mashirika hayo kujitegemea.

Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali uliofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimatiafa cha Arusha (AICC).

Amesisitiza kuwa safari ya mageuzi kwenye Mashirika ya Umma inaendelea na kwamba tayari matokeo chanya yameanza kuonekana ikiwemo kuongezeka kwa mapato, hali ya kujiamini ndani ya Mashirika na katika ubunifu wa watendaji.

Aidha, ametolea mifano ya Mashirika kadhaa, ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo limeweza kuongeza umiliki wake wa Kitalu cha gesi asilia cha Mnazi Bay kutoka 20% hadi 40%, na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira-Tanga (Tanga-UWASA) kutumia Hati Fungani (Bond) kupata jumla ya Shilingi Bilioni 54.72 kama njia mbadala ya kupata mtaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji na utunzaji wa mazingira.

Rais Dkt. Samia pia ameyataka Mashirika kupunguza utegemezi serikalini kiuendeshaji, akitolea mfano wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambalo kufuatia mageuzi limeanza kupata faida na kuanza kulipa mishahara ya watumishi wake.

Hali kadhalika, amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma kuimarisha utamaduni wa uwajibikaji na kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma. Pia, amesisitiza umuhimu wa Mashirika ya Umma kufanya utafiti wa kutosha kuhusu uwekezaji ili kukwepa kutumia fedha za walipa kodi bila matokeo.

Katika tukio lingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua na kukabidhi ndege za mafunzo za Marubani namabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyikakatika Kikosi cha Usafirishaji jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho yamiaka 60 ya JWTZ.

Amtimshia Kobe mwajiri wake ili alipwe mshahara
Katimba: Kipaumbele ni ujenzi miundombinu ya Msingi