Mwanamke mmoja raia wa Zimbabwe, Sithembiso Budzirikawa (58), anashikiliwa na vyombo vya usalama baada ya kudaiwa kumtishia Meneja wake kwa uchawi, ili alipwe mshahara wake.

Mwanamke huyo anadaiwa alienda shamban!i ili kumpata kobe na kuenda naye kazini akiwa amemfunika kwa kitambaa chekundu na kumzungushia sindano kisha kumkabili meneja wake huyo ambaye alimtuhumu kumcheleweshea stahiki.

Kufuatia tukio hilo, Meneja alitoa taarifa Polisi ambao walifika na kumuomba Mwanamke huyo kibali cha kobe ambacho hakuwa nacho hivyo kukamatwa chini ya sheria ya hifadhi ya wanyamapori kwa kumiliki kobe hai kinyume cha sheria.

Budzirikawa alifikishwa mahakamani, ambapo alipatikana na hatia na alihukumiwa kulipa faini ya dola 300 za Kimarekani au kifungo cha siku 30 jela.

Azam FC yamweka kikaangoni Dabo
Mashirika ya Umma yaendelee kusimamia mageuzi - Rais Samia