Huduma ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imepungua kutokana na hitilafu ya umeme katika mfumo wa kupokea umeme kwenye mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam – DAWASA, imeyataja maeneo yanayoathirika kuwa ni Mlandizi, Msufini, Vigwaza, Chamakweza, Ruvu, Kwa Mathias, Pangani Bokomnemela, Kibaha, Visiga, Picha ya Ndege, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Makabe.
Maeneo mengine ni Kimara, Msewe, Changanyikeni, Mabibo, Kisarawe, Ukonga, Kinyerezi, Tabata, Temeke, Segerea, Makuburi, Ubungo Maziwa, Mwananchi, Kiwalani, Lumo, Yombo Vituka, Uwanja wa Ndege, Banana, Viwanda vya Barabara ya Nyerere, Jet, Buguruni na TAZARA.
DAWASA pia imeeleza kuwa Wataalam wa DAWASA na TANESCO wanashirikiana, ili kurudisha huduma katika hali ya kawaida na kuwaomba wananchi waishio katika maeneo hayo kuwa wavumilivu.