Askofu wa Jimbo katoliki la Musoma, Mhasham Michaely Msonganzila amewataka Watanzania kuendelea kudumisha Amani na upendo, wakati hu ambapo Taifa lipokatika maandalizi ya uchaguzi wa Serikali ya mitaa 2024.
Askofu Msonganzila amesema hayo Wakati akizungumza na waandishi wa Habari Nyumbani kwake Jimbo katoliki la Musoma kwenye Maandalizi ya kuelekea jubilee ya miaka 40 ya upadre wake ambayo ilifanyika Tarehe 29.08.2024 Jimbo katoliki la Musoma.
Amesema, amani ni tunu kubwa inayopaswa kutunzwa na kila mtu hivyo viongozi watakao wania nafasi mbalimbali za uongozi muhimu kuhubiri amani ya kweli na kuacha kukumbatia uongo ambao una madhara makubwa kwa Taifa.