Afisa Mwandikishaji Jimbo la Babati Mjini, Edna Moshi amefungua rasmi mafunzo kwa waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi katika Shule ya Sekondari Babati Day Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura litaanza tarehe Septemba 4 – 10, 2024 katika Vituo takribani 64 vilivyopo ndani ya Kata nane.

Mafunzo hayo, yameudhuriwa na Mariam Kiravu Afisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Msimamizi wa Mkoa wa Manyara,Wataalam wa TEHAMA kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Aro Jimbo na Aro Kata, Mwenyekiti wa Mafunzo, Wakufunzi wa Mafunzo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ugavi.

Edna amesema takribani Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa vifaa vya Bayomertiki 158 wamepatiwa mafunzo ambayo yanalengwa kuwajengea umahiri zaidi na ndio wahusika wa uandikishaji wa wapiga kura vituoni.Na kuwasisitiza kuvitunza vifaa ambavyo watakabidhiwa wakati wa zoezi hilo na kufanya kazi kwa umakini vituoni.

Edna amesema kuwa katika uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhuiswa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura lakini mawakala au Viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kituoni.

Aidha ameongeza kuwa Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa Uboreshaji wa Daftari kwa Asasi za kirai 157 na asasi 33 za kirai kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo.

Dkt. Posi: Shirikianeni kuishauri Serikali uendeshaji wa mashauri
Mbappe:Ukata wa mabao sasa basi