Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS), wametakiwa kushirikiana kutekeleza majukumu yao kwa wakati, ili kufikia malengo waliyojiwekea ndani ya muda uliopangwa.

Wito huo umetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati wa kikao chake cha kwanza na Menejimenti ya Ofisi hiyo, tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Prisca Ulomi  imesema malengo ya kikao hicho ni kufahamiana, kuwekana sawa na kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo, Dar es Salaam.

Wakili MKuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutoa mwelekeo wa Ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Dar es Salaam.

“Tufanye kazi kwa ushirikiano kwa muda wote, mtu anapokwama apewe ushirikiano, tusing’angianie tu kanuni za utumishi, ila haimaanishi tuvunje kanuni na taratibu za Serikali, tupunguze kufuata milolongo isiyo ya lazima ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati na kubadilika badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” amesema Dkt. Posi.

Ameongeza kuwa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imekasimiwa majukumu ya kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake hivyo amewataka wajumbe wa Menejimenti kuishauri Serikali kwa wakati kuhusu uendeshaji wa mashauri mbali mbali, ili kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za uendeshaji wa mashauri na ulipaji wa fidia.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kikao chake na menejimenti hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, ametoa wito kwa menejimenti hiyo kuzingatia mawasiliano kwa kuwa mawasiliano ni muhimu, mawasiliano yafanyike kwa wakati na watoe mrejesho wa hatua za utekelezaji wa majulcumu, na wazirtgatie mnyororo wa kufanya maamuzi kwa lcuwa ni muhimu ndani ya Serikali.

Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Alice Mtulo akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ofisi hiyo kwa Dkt. Possi ameahidi kurnpa ushirikiarto na kutekeleza maelekezo na miongozo yote aliyoitoa ili kuongeza tija na ufanisi katilca kuhudumia wananchi na kuiwakilisha Serikali na taasisi zake katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi ndani na nje ya nchi.

Serikali yataka magonjwa ya mlipuko yadhibitiwe
Babati: Mafunzo uboreshaji Daftari la wapiga kura yafunguliwa