Klabu tatu za Uturuki , Fenerbahce, Besiktas na Eyupspor zote zina nia ya kumsajili mlinzi wa Newcastle Kieran Trippier baada ya klabu ya Saudi Pro League Al-Ittihad pia kujaribu kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, 33. (Sky Sports)

West Ham wanavutiwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Joel Matip, 33, na mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland John Egan, 31, huku wakitafuta soko la wakala huru kumnunua beki mpya wa kati. (Sky Sports)

Manchester United haiwezi kumruhusu kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 32 kuondoka mwezi huu. (Football Insider)

Newcastle itajaribu tena kumsajili winga wa Nottingham Forest mwenye umri wa miaka 22 kutoka Sweden Anthony Elanga katika dirisha dogo la usajili. (Football Insider)

Ajax wamekubali kwa mdomo mkataba wa mkopo na Southampton kwa mshambuliaji wao wa miaka 22 wa Ghana Kamaldeen Sulemana. (Fabrizio Romano)

Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu beki wa kati wa Palmeiras mwenye umri wa miaka 18, Mbrazil Vitor Reis. (Caughtoffside), nje

Everton ilikataa nafasi ya kumsajili mlinzi wa Chelsea Axel Disasi, mchezaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, na fowadi wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21, katika makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa Toffees Dominic Calvert-Lewin, 27. (Givemesport )

Winga wa Manchester City Mwingereza Joel Ndala, 18, anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na PSV Eindhoven kwa mkopo ikiwa na masharti ya kununua. (Athletic – Subscription Required)

Mshambuliaji wa Romania Ianis Hagi, 25, anatazamiwa kukataa nafasi ya kuondoka Rangers na kujiunga na Bucharest FCSB. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Scotland Stuart Armstrong, 32, ambaye aliondoka Southampton mwishoni mwa msimu uliopita, anakaribia kuhamia Vancouver Whitecaps. (Daily Hive

Makala: Uchaguzi wa Abiria na mashaka ya safari
Mkutano FOCAC: Rais Samia awasili China