Inasadikika kuwa Komba ndiye Mnyama mlevi kuliko wanyama wote ambaye pia akilewa hulia bila sababu na ukimuona sura yake imekaa kilevi akipendelea zaidi pombe za kienyeji.

Kimuonekano ni mnyama jamii ya Kima na ni mdogo kuliko wote akipendele kutembea usiku pekee kwani mchana analala na watu wamempachika jina la Bush baby na muda mwingi wa Maisha yake anatumia akiwa juu ya mti.

 

Ana macho makubwa yanayomsaidia kuona wadudu gizani na masikio makubwa yanayomsaidia kusikia vizuri akiwa na umbo dogo ingawa analia kwa sauti kubwa inayofanana na ya mtoto, mkononi akiwa na vidole vitano na kucha kama za mtoto na ndiyo sababu wanamuita Bush baby.

Chakula chake kikuu ni matunda na wadudu lakini maajabu anakunywa pombe ya mnazi maarufu kama tembo halafu mara nyingi hufa akiwa juu ya mti kamwe huwezi kumuona kafia ardhini labda awe amegongwa au kapigwa na anaishi miaka 3 Hadi 4.

Taifa Star: Tuko imara kuwakabili Waethiopia
Suarez atoa neno la mwisho Uruguay