Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli, Francois Adelaide amesema Jeshi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, limekuwa msaada mkubwa kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika.

Adelaide ameyasema hayo Septemba 3, 2024 walipotembelea Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma na kuongeza kuwa wanathamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika.

Amesema, nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati hiyo kwa utambuzi wa mchango wa JWTZ.

Bunge lapokea taarifa ya Kamati ya Sheria
Manchester United yamkacha nyota wake