Johansen Buberwa – Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani limepokea taarifa ya kamati ya sheria inayo husu mjadala wa uchambuzi na utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sheria ndogo katika mkutano wa 16 kwenye kikao cha saba.
Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kwenye kikao cha bungeni jijini Dodoma Septemba 4, 2024 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Jasson Rweikiza amesema walifanya udadisi kama hakutakuwepo utekelezaji wa maazimio yakipitishwa na kufanyiwa marekebisho kwa ngazi ya Wizara.
Amesema jambo jingine ni maazimio ya kupelekwa kufanyiwa marekebisho kwa mwanasheria mkuu wa serikali na kuhakiki yakiwa na lengo la kufikia hatua inayolenga kulinganisha na hatua inayosohili ili kulishauri bunge kwenye uamuzi unaofaa na hatua zilizoripotiwa kwa kusahihisha dosari.
Dkt. Rweikiza amesema kipimo kikuu kilichotumika ni kufuata Mashariti ya katiba kupitia sheria mama na za nchi ambapo kamati hiyo ilenga kujiridhisha na mambo makuu matano.
“Moja iwapo sheria ndogo zinapingana na katiba mbili iwapo sheria ndogo zinamashariti kupingana na sheria mama na sheria nyingine za nchi tatu iwapo sheria ndogo zinamakosa kwa kutoendana na misingi ya uhandishi nne iwapo sheria ndogo zinamashariti yasiyo na ualisia kwa kiasi cha kusababisha changamoto katika utekelezaji wake na tano iwapo sheria ndogo zina majeduari yenye dosari kama kutofautiana vifungu vya sheria ndogo vinavyo anzisha,” amesema Dkt. Rweikiza.
Tathmini imeonesha hadi kufikia Agosti 23 mwaka 2024 sheria ndogo 19 zilikuwa zimefikia hatu ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali kupitia wizara ya Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji,habari na teknoloknolojia,Wizara ya kilimo,Wizara ya Nishati,Ofisi ya Waziri Mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Wizara ya Viwanda na Biashara Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi na Wiza ya Maji.
Baadhi ya Wabunge waliotoa michango yao kwenye kikao hicho akiwemo Amida Abdallah, Mariam Omary na Tarimo wemesema wamejifunza mambo mengi na ya muhimu kuhusu sheria ndogo hasa utekelezaji wa kila siku katika shughuli za kiserikali.
Wamesema ni lazima yazingatie sheria na kanuni na miongozo mbalimba ambayo nchi imeweka, ili kuharakisha kupata maendeleo na kuleta ustawi wa wananchi ndani ya Taifa hilo pamoja na kuongeza ajira katika sekta binafsi.
Kwa upande Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema sheria hizo tayari zimesha hakikiwa na tayari zimetangazwa kwenye gazeti la serikali kwa matoleo mawili la kwanza ni kwanjia ya kingereza kupitia GN namba 677 na toleo la kiswahili namba GN 679 na kanuni zikitarajiwa kutolewa tarehe 05 Septemba 2024 kwenye gazeti la serikali.
Naibu Spika wa Bunge, Hassan Zungu meelekeza kwa kwa sheria ndogo ambazo zinadosari zilizoelekezwa na kamati ya Sheria zilekebishwe na kufanyiwa kazi na kufika mwezi Desemba Mwaka huu ziwe zimewasilishwa Bungeni.