Mwanafunzi mmoja (14), amewauwa watu wanne kwa risasi katika shule ya Sekondari ya Apalachee huko Georgia nchini Marekani na kusabahisha majeruhi tisa na taharuki miongoni mwa Wanafunzi wengine wa Shule hiyo.

Waliouawa ni Wanafunzi wawili na Walimu wawili, huku majeruhi hao wakikimbizwa Hospitalini ambapo mshukiwa ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo akijisalimisha na kuwekwa chini ya ulinzi.

Inaarifikwa kuwa mwanafunzi huyo aliwahi kuhojiwa na shirika la upelelezi la Marekani – FBI, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mtu asiyejulikana Mei mwaka 2023 kuhusu vitisho vya mtandaoni vya kufanya shambulio la risasi shuleni.

Tayari wagombea urais wa Taifa hilo, Kamala Harris na Donald Trump wameeleza kusikitishwa kwa na tukio hilo na kutoa pole kwa wafiwa, majeruhi na kusema vyombo vya dola vitatimiza wajibu wao.

Tetesi za usajili Duniani leo 05 septemba 2024
DRC: Matumaini yatawala kuwasili kwa chanjo ya Mpox