Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni nguzo muhimu katika afua za afya, Ustawi wa Jamii na Lishe.

Dkt. Kapologwe amebainisha hayo katika Kikao Kazi cha Kuandaa Mpango wa Kuharakisha Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya  Ngazi ya Jamii nchini ambacho kimekutanisha Wadau wa sekta ya Afya kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani  kwa kushirikiana na  Shirika la Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa la Afrika (Africa CDC) pamoja na Wadau wengine .

Amesema, “Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanatusaidia sana ikiwemo kupita kaya kwa kaya kutoa elimu ya afya na kudhibiti magonjwa hayo, ni Ngazi ya Jamii wamekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa taarifa kuhusu magonjwa ya mlipuko ambapo amesema ni askari na nguzo muhimu katika mapambano ya magonjwa ikiwemo utoaji wa elimu ngazi ya Jamii.”

Akizungumzia umuhimu wa ushirikiano  katika utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii huku lengo la Kikao hicho likiwa ni kujadili masuala ya Uratibu  kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii na  kupendekeza utaratibu ambapo wadau wanaotekeleza afua zinazohusiana na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wataweka  Mipango ya Utekelezaji.

Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ulizinduliwa tarehe 31, Januari, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Kikao hicho kimehusisha Watalaamu kutoka Wizara ya Afya (Bara na Visiwani), Ofisi ya Rais  TAMISEMI, Africa CDC, UNICEF, USAID, IRISH AID, Wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU)  na Wadau mbalimbali ambapo kimeanza  Septemba 3, 2024 hadi Septemba 6, 2024 Jijini Dar es Salaam

Majaliwa: Tanzania itaendelea kujiimarisha Kidiplomasia
Mazingira: Viwanda viwe na mifumo ya majitaka - Dkt. Kijaji