Wachezaji kumi wa Premier League wameteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2024.Kwa jumla, vilabu vinne vya Ligi Kuu vina angalau mchezaji mmoja anayewania tuzo hiyo, baada ya orodha ya wachezaji 30 kutangazwa siku ya  Jumatano.

Arsenal na Manchester City zinaongoza kwa kuwa na wachezaji wanne kila moja, Martin Odegaard, Declan Rice, William Saliba na Bukayo Saka kutoka Gunners, huku Ruben Dias, Phil Foden Erling Haaland na Rodri wakitambuliwa kutoka kwa Mabingwa wa sasa wa Ligi Kuu ya Uingereza Man City.

Nyota wa Chelsea Cole Palmer pia yuko kwenye orodha ya walioteuliwa, pamoja na mlinda mlango wa Aston Villa Emiliano Martinez.Wateule hao watakuwa wakitafuta kuwa mchezaji wa tatu pekee wa Premier League kushinda tuzo hiyo, baada ya Michael Owen wa Liverpool mwaka 2001 na Cristiano Ronaldo kwa Man Utd mwaka 2008.

Washindi watatangazwa wakati wa hafla ya tarehe 28 Oktoba katika Ukumbi wa Theatre du Chatelet huko Paris. Emiliano Martinez pia ametangazwa kuwania tuzo maalumu ya  Yashin Trophy, inayotunukiwa kwa golikipa bora na hii ni mara ya pili mfululizo kwa mchezaji huyo.meneja wa Man City, Pep Guardiola ameteuliwa kuwania tuzo ya Kocha Bora wa Timu ya Wanaume.

Wachezaji wawili wa Manchester United, Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo, pamoja na winga wa Man City, Savinho, wameteuliwa kuwania Tuzo ya Kopa, inayotolewa kwa mchezaji bora chini ya umri wa miaka 21. Tuzo hiyo ilinyakuliwa na beki wa sasa wa Man Utd Matthijs de Ligt mwaka 2019 alipokuwa akiichezea Juventus.

Man City pia ni moja ya klabu tano zilizoteuliwa kuwania tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka ya Wanaume, tuzo ambayo wanatazamia kushinda kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Shambulio la risasi: Bob Wine kufanyiwa upasuaji
Si Ronaldo wala Messi tuzo za Ballon d'or