Tai anapojenga kiota chake, hukusanya matawi yenye miiba na kuyatumia kama msingi wa kiota halafu baadaye hukusanya manyoya laini, ili kufunika miiba.
Mtoto wa Tai anapokuwa na umri wa kuweza kuruka lakini amelegea sana kwa sababu ya raha za manyoya laini ya kwenye kiota, mama Tai huondoa manyoya, ili mtoto apate maumivu ya miiba na ajue ni wakati wake wa kuondoka kwenye kiota na kuruka.
Ipo hivi: MUNGU anapotaka kukusogeza mahali pa juu zaidi, ataondoa manyoya laini ya eneo ulilopo ili upate maumivu ya miiba na uchungu.
Kusudi la Mungu ni kukupeleka mapambano na sio kukudhuru, hivyo kitendo kama hicho kinaashiria au kukujulisha kuwa ni wakati wa kuondoka ili kwenda kupambana ili kusudi lako maishani litimie.
Jipe moyo unapokabili magumu maishani. Wakati wowote maumivu yanakuja, jaribu kuyavumilia maana ni njia ya MUNGU ya kukuambia uondoke kwenye raha ya muda ili upae hadi viwango vya juu.