Nchi za Afrika zimetakiwa kuunganisha nguvu na kubuni na kutumia rasilimali na vyanzo mbalimbali vya nishati  vilivyopo kuchochea maendeleo ya uchumi endelevu, kwa kuweka mifumo na sera za kuwezesha matumizi ya teknolojia na mbadala.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko jijini Windhoek Nchini Namibia wakati akihutubia Mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi ya Hydrogen kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme.
Amesema, nchi hizo za Afrika kuifanya ajenda ya nishati safi kuwa ya pamoja miongoni mwa nchi hizo ambayo inapunguza gharama za uedeshaji na kupungguza changamoto za kiafya na kwamba tayari Tanzania inatekeleza mkakati wa upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa gharama nafuu, hali inayochochea maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa,  pamoja na changamoto za kifedha, miundombinu na masoko katika matumizi ya Hydrogen, lakini ushirikiano na uhusiano mzuri miongoni mwa nchi za Afrika linaweza kuwa suluhisho Tanzania itaendelea kuwa kinara katika matumizi ya Nishati safi kwa kushirikiana na mataifa mengine ya Afrika katika kupitia mifumo, miundo sera na sheria zinazolenga katika maendeleo endelevu.
Mkutano huo umefunguliwa na  Makamu wa Rais wa Nchi hiyo, Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye amewataka washiriki kutumia fursa ya mkutano huo kuanisha mbinu na mkakati unaoweza kutumika kuleta maendeleo ya nchi husika kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Amesema Namibia inajivunia matumizi ya Hydrogen kwa matumizi ya viwanda kwa manufaa nchi hiyo, nchi Jirani pamoja na mataifa mengine yaliyo katika mlengo wa matumizi ya nishati hiyo.
Tayari Tanzania ipo katika hatua za awali katika kuendeleza matumzi ya Hydrogen hivyo inatumia fursa ya Mkutano huo kujifunza kuhusu fursa na Changamoto zinazoweza kujitokeza ambapo kwa nchi za Afrika ambazo zinatumia Hydrogen ni pamoja na Namibia, Afrika Kusini, Kenya, Maouritania na Morocco.

Majaliwa atoa maelekezo uendeshaji Mradi SGR
Huu hapa uwanja mpya wa Inter Miami