Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Maputo, Msumbiji akitokea nchini Indonesia kwa gwaride maalum na ujumbe wake akiwemo Mkewe Mama Mariam Mwinyi.
Katika uwanja wa ndege wa Maputo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji akiwemo Waziri wa Afya wa nchi hiyo.
Dkt. Mwinyi atashiriki Sherehe za Miaka 50 ya Siku ya Ushindi nchini Msumbiji ambapo kuhudhuria kwake katika sherehe hizo kunatokana na mualiko Maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi.