Takriban watu 48 wamefariki baada ya Lori la mafuta kugongana na gari nyingine kisha kulipukq katika jimbo la Niger lililo eneo la kati, la kaskazini mwa Nigeria.
Lori hilo la mafuta liligongana na lori lililokuwa linasafirisha watu na mifugo na kupelekea magari mengine mawili, kuhusika katika ajali hiyo na kuwaka moto.
Msemaji wa idara ya majanga, Hussaini Ibrahim alisema idadi ya waliofariki ni 48 huku Maafisa wakiweka jitahada za kuondoa magari hayo kwenye eneo la tukio.
Kampuni ya mafuta inayomilikiwa na Serikali NNPC hivi karibuni iliongeza bei ya petroli kwa asilimia 39, ikiwa ni ongezeko kubwa la pili kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini uhaba wa mafuta umeendelea.