Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze, Hassan Mwinyikondo ametoa siku sita kwa Mamlaka ya Maji Safi na maji taka DAWASA Wilayani humo kuhakikisha wanamaliza tatizo la kukosekana kwa maji ikiwemo Kata ya Msoga.

Agizo hilo, amelitoa wakati akihitimisha ziara ya kuhimiza maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji Kata ya Msoga kwenye mkutano Mkuu wa Kata ambapo kero ya ukosefu wa maji iliibuliwa na Wananchi.

Amesema, DAWASA wamekosea kukata mabomba yaliyowekwa kwenye vioksi vya kuuza maji na kusababisha kukosekana kwa uhakika wa huduma ya maji ya Bomba kwa wananchi wa Halmshauri ya Chalinze.

“Tumepokea kero ya huduma ya maji katika Kata na vijiji vyote vya Chalinze tukiwa kwenye ziara zetu za kazi vijijini hivyo sekta ya maji Jimbo la Chalinze wanaweza wakatumaliza, bila kusimamia utekezaji wa madhubuti wa sekta ya maji wanaweza wakatumaliza,” alisema.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Halmshauri ya Chalinze aliomba Mkutano maalumu na Mameneja ya sekta ya huduma za maji wa DAWASA na Mamlaka ya Maji vijijini RUWASA ili wakae kujadiliana kwa pamoja waone chakufanya ili kumaliza kero hiyo ya huduma ya maji Chalinze kwa pamoja.

Akijibu kero na changamoto hizo za Wananchi Afisa Maji wa DAWASA Kata ya Msoga, Muhsini Msisi amesema tayari wameshughilikia sehemu kubwa ya kero hizo ambapo kwasasa wapo katika hatua ya kujaza maji kwenye matanki Kisha wafungulie maji yawafikie Wananchi.

Mkutano huo, pia ulitanguliwa na mkutano wa ndani wa Wana CCM ambapo Mwenyekiti huyo ambaye pia ndio Diwani wa Kata ya Msoga alihimiza umuhimu wa kufanyika vikao vya Chama na Jumuiya zake kujenga uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM hasa kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji.

Babati: Mpendu awaita Wananchi kujiandikisha, kuboresha taarifa
Mlipuko Lori la mafuta wauwa 48