Anaitwa Ladi Kwali (1925 – 1984), ni Mwanamke ambaye anaoneka kwenye noti ya naira ishirini ya Nchini Nigeria.

Mwanamke huyu alizaliwa katika kijiji cha Kwali, kilichopo eneo la Gwari Kaskazini mwa Nigeria, ambapo ufinyanzi ulikuwa kazi ya kawaida miongoni mwa wanawake.

Alikuwa na ustadi sana hivi kwamba kazi yake ilijulikana huko Uropa, Uingereza na Amerika. Mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya 1960 na kazi zake ilioneshwa London katika Matunzio ya Berkeley.

Alikua mfinyanzi anayejulikana zaidi wa Nigeria, akatunukiwa udaktari na akafanywa MBE mwaka 1963 licha ya kutokuwa na elimu rasmi, hakika ujuli ulimlipa na heshima akaipata.

Mbowe: Iundwe kamati kushughulikia matukio ya utekaji
Msiba kada wa CHADEMA: Kelele zaibuka, hotuba yakatishwa