Mwanasheria Mkuu wa Yanga Simon Patrick ametema nyongo juu ya kilichofanywa na mchezaji wa Simba, Kiungo Yusuph Kagoma ambaye alisajiliwa na Yanga kwa mujibu ya taarifa kutoka klabuni hapo.Hadi sasa inaelezwa kwamba Yanga wamemtaka mchezaji huyo kuomba msamaha hadharani, kwa kile alichokifanya tofauti na hapo hatua zaidi za kisheria zitafuatwa.

“Kanuni ya 41 (13) ya Kanuni za Ligi Kuu ya 2024/2025 inasema kuwa mchezaji atakayebainika kusaini mikataba na timu zaidi ya moja atafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka 1 hadi 3.

“Kwenye ligi ya Cuba, kuna mchezaji mwenye mikataba miwili, na tayari ameshacheza mechi mbili za ligi.

“Tathmini ya haraka inaonyesha kuwa pale kanuni zinapozigusa timu, wadau wengi hukubaliana kwamba ni njia sahihi ya kukuza soka letu, lakini zinapowagusa wachezaji, wadau hubadilika kuwa kama walezi au wazazi, wakisisitiza matumizi ya busara kwa hoja kwamba maisha ya mchezaji ni mafupi.”

“NB: January na mimi nitasaini vilabu viwili alafu nitacheza timu nitakayoamua.- Alimalizia kwa kuandika hivyo Wakili Simon Patrick.

Magoma na Mwaipopo wakalia kuti kavu kesi na Yanga
Mwamnyeto Foundation yamgusa Mdamu