Hili ni Jiwe kubwa zaidi kuwahi kuchongwa na mwanadamu, likifahamika kama Jiwe la Mwanamke Mjamzito.

Linapatikana eneo la Baalbek, huko Nchini Lebanon ikiaminika kuwa ilichongwa karibu karne ya kwanza K.K., ikiwa na urefu wa takriban mita 21.5 (futi 70.5), upana wa mita 4.8 (futi 15.75) na urefu wa mita 4.2 (futi 13.8).

Jiwe hili lina uzito wa takriban tani 1,000 hadi 1,200 (pauni 2,000,000 hadi 2,400,000 au kilo 907,185 hadi 1,088,622) na watu hutembelea eneo hilo kama sehemu ya utalii.

Jiwe la Mwanamke Mjamzito, linaangazia uwezo wa kushangaza wa wahandisi wa zamani ambao walifanya mambo makubwa yaliyoacha historia isiyofutika.

Ukubwa wa jiwe hilo ni ni wa kushangaza sana kiasi kwamba ikazuka maswali kwanini upande mmoja ulididimia na niji kusudio la mchongaji, huku uendelevu na ustadi wa ajabu wa waundaji wake ukiendelea kushangaza hadi hii leo.

Skanka Tani 1.8 zadakwa, Watano mbaroni
Mafuriko yauwa 341, UN yatoa tahadhari