Katika pango hili kuna utata wa mabaki ya mabaki ya Mwanamke yaliyopatikana baada ya miaka 34,000.
Pango hilo linatazamana na Bahari lakini miaka 34,000 iliyopita haikuwa rahisi kulifikia, na ufikiaji wake uliwezekana wakati ambao mawimbi yanakuwa ya kiwango cha chini.
Mnamo mwaka 1823, Profesa Buckland wa Chuo Kikuu cha Oxford aligundua sehemu ya mifupa ndani ya Pango hilo la Paviland.
Mifupa hiyo, ilikuwa na rangi nyekundu na kitu kama mkufu uliotengenezwa kwa vipande vya jumba la konokono wadogo na pembe za ndovu ulipatikana maeneo ya shingoni.
Buckland aliamini kuwa mabaki hayo yalikuwa ya Mwanamke na alimpa jina la The Red Lady of Paviland.
Hata hivyo, baadaye ikaja kujulikana kuwa mifupa hiyo ni ya kijana mwenye umri wa miaka ishirini ambaye alizikwa miaka 34,000 iliyopita KK.
Pango la Paviland ni muhimu katika historia kutokana na mazishi ya kwanza yanayojulikana sio tu nchini Uingereza bali pia katika Ulaya Magharibi.
Linapatikana karibu na Pilton Green, Swansea, huko Wales.