Serikali Nchini, itaendelea kuhakikisha ustawi wa Wauguzi, Madaktari na Watumishi wote wa Sekta ya Afya wanapata stahiki ikiwemo kuwasimamia na kufuatilia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao huku ikiwasihi  kuwa na lugha zenye staha kwa Wagonjwa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama hii leo Septemba 11, 2024 wakati akiongea na Watumishi na Wagonjwa akiwa kwenye ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Moyo ya Jakawa Kikwete – JKCI, Jijini Dar Es Salaam.

“Afya ni usalama wa nchi, Afya ni maendeleo ya nchi, Afya ni jambo la msingi sana katika ustawi wa Taifa, tunasema leo tumefikia uchumi wa kati ni kwa sababu tumeboresha Afya za wananchi kwa hiyo ni lazima tusimamie vizuri maslahi ya watumishi lakini na utendaji wao.” Amesema Mhagama.

Aidha, amesema Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa katika Sekta ya Afya hasa katika uwekezaji wa rasilimali watu pamoja na vifaa, vifaa tiba katika huduma za ubingwa bobezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete – JKCI, Dkt. Peter Kisenge amesema Taasisi hiyo kupitia Samia Outreach Program imeweza kufikia mikoa 16 na wananchi elfu 17,000 wamewaona na wengine na Taasisi hiyo kwa matibabu.

“Kila siku katika Taasisi yetu tunafanya upasuaji kwa wagonjwa Wanne hadi Watano na tunawaona wagonjwa mia 500 kwa siku Moja, vilevile tumeimarisha tiba utalii ambapo tunawaona wagonjwa mia 343.” amesema Dkt. Kisenge.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 12, 2024
Zaidi ya Kilo 13 za Dhahabu zadakwa zikitoroshwa, watatu mbaroni