Watanzania wahimizwa kujitoa kuwekeza kwenye Huduma za kuwasaidia waraibu wa Dawa za Kulevya kwa kuanzisha nyumba za upataji nafuu Ili kuokoa nguvu kazi ya taifa ilipotea kwenye dibwi la matumizi ya Dawa haramu za Kulevya.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma na kusisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya vituo hivyo ili kukabiliana na tatizo la uraibu wa dawa za kulevya nchini.

Amesema, “tunahitaji Sobar houses zaidi, hasa katika maeneo ambayo huduma hii haipatikani kwa urahisi,” alisema Lyimo. “Idadi ya wateja wa dawa za kulevya nchini ni kubwa kuliko uwezo wa vituo vilivyopo sasa hivi.”

Kamishna Jenerali Lyimo amewataka wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Soberhouses) kuhamasisha wenzao kufungua vituo vipya, akibainisha kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kuchangia katika juhudi za kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.

“Kufungua Soberhouse sio lazima uwe umewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya. Muhimu ni kufuata taratibu zilizowekwa na serikali,” aliongeza.

Kwa upande wao, wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses) wameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, ikiwemo ukosefu wa utambuzi na rasilimali za kutosha.

Mwenyekiti wa mtandao huo, Hamisi Shuwira, aliomba serikali kutoa vitambulisho vya utambuzi kwa wamiliki wa Sobahouses ili kurahisisha kazi yao ya kuwasaidia wateja.

Naye Katibu wa mtandao huo, Saidi Bandawe, alisema ni muhimu kwa wamiliki wa Soberhouses kufuata taratibu zilizowekwa na kutoa taarifa za mara kwa mara. Aliongeza kuwa kupambana na uraibu wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania, si serikali pekee.

Wiki ya Polisi: Kikosi chazindua upimaji afya bure
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 12, 2024