Newcastle wanamfanya Angel Gomes kuwa mlengwa wao mkuu, Galatasaray wanajiandaa kutoa ofa kwa Emerson Palmieri, Wesley Fofana anafikiriakuihama Chelsea na kujiunga na Marseille msimu huu wa joto.

Kiungo wa kati wa Uingereza na Lille Angel Gomes amekuwa akitajwa kuwa ni mlengwa mkuu wa Newcastle , lakini Liverpool , Tottenham na Borussia Dortmund pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.(Sun)

West Ham wanajiandaa kupokea ofa kutoka kwa Galatasaray kwa ajili ya beki wa Italia Emerson Palmieri, 30. (Football Insider)

Beki Mfaransa Wesley Fofana, 23, anasema alifikiria kuondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya nyumbani ya Marseille msimu huu wa joto. (Free Foot – kwa Kifaransa), nje

Manchester City , Chelsea na Liverpool wanavutiwa na kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Chris Rigg, 17. (Givemesport)

Mauricio Pochettino, 52, atapokea mshahara wa kila mwaka wa karibu $6m (£4.6m) kama meneja wa Marekani . (ESPN)

Shirikisho la soka England limezungumza na baadhi ya wasimamizi wengine licha ya kipindi cha faraja cha Lee Carsley hadi sasa kama kocha wa muda wa England. (Telegraph – usajili unahitajika)

Meneja wa zamani wa England Gareth Southgate, 54, anasema kazi yake inayofuata inaweza kuwa tofauti na soka. (Sky News)

Fifa iko kwenye mazungumzo ya kupanua Kombe la Dunia la Wanawake hadi timu 48 mapema kufikia 2031, kulingana na ukubwa wa mashindano ya wanaume. (Telegraph – usajili unahitajika)

th

Chanzo cha picha,Getty Images

Tottenham , Newcastle na Arsenal wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 24, ingawa Juventus pia wanavutiwa naye. (TuttoJuve)

Chelsea na Tottenham bado wanavutiwa na mlinzi wa Lecce wa Denmark Patrick Dorgu, 19, ambaye thamani yake ni takriban euro 40m (£33.8m). (La Gazzetta dello Sport kupitia SportWitness)

Mlinzi wa Monaco na Brazil Vanderson, 23, ameivutia sana Chelsea , huku Manchester United na Tottenham pia wakimtaka nyota huyo(Caughtoffside)

Singida BS yapania kumtoa Simba kileleni
Yanga yawasili Ethiopia kwa mafungu