Vijana wengi duniani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo elimu duni na ukosefu wa ajira, hali inayowasababisha kukosa matumaini, kujiingiza katika uhalifu, kuandamana mitaani na kuhama nchi zao kwa kutafuta maisha bora.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Septemba 12, 2024 na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani – IPU, Dkt. Tulia Ackson wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 10 wa Wabunge Vijana wa IPU unaofanyika Jijini Yerevan, nchini Armenia.

Amesema, katika nyakati hizi zenye misukosuko duniani mahitaji ya vijana hayapaswi kupuuzwa. Amehimiza Viongozi na Wabunge kuhakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa vijana na kuwapa kipaumbele katika kupata elimu bora na fursa za ajira.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinyan na  kuhudhuriwa na Viongozi wa Mabunge na Wabunge Vijana kutoka nchi Wanachama wa IPU.

Maisha: Serena, Venus Williams walivyomtoa meno baba yao
Sitajishusha kwa Davido mimi ni tajiri kuliko yeye - Portable