Klabu ya Yanga imeendelea kusisitiza uhalali wa mchezaji Yusuf Kagoma anayekipiga Simba. Klabu hiyo kupitia mwanasheria wake Simon Patrick imeendelea kusisitiza kwamba kagoma alikwishasaini mkataba na Yanga na hapaswi kutumikia timu nyingine . Mwanasheria huyo amesisitiza kwamba Shauri la kimkataba lipo katika kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji na kama litasikilizwa basi mchezaji huyo atajiweka katika wakati mgumu.Simo Patrick ameyasema hayo wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na alionyesha mkataba wa mchezaji huyo amba alisaini na Yanga.
“Yanga Sc ilimnunua Yusuph Kagoma kutoka Singida Fountain Gate Fc kwa thamani ya milioni 30 na Malipo yao yalikuwa kulipa kwa awamu na Malipo hayo tulifanya kwa wakati na huyo mchezaji ni halali kuwatumikia Yanga SC.Mpaka sasa tumewalipa Singida Fountain Gate Fc shilingi milioni 60 zikiwa na mchanganuo kwa wachezaji wawili ambao ni Yusuph Kagoma milioni 30 pamoja na Fedha za Nickson Kibabage milioni 30 ambazo zilikuwa ni deni”Mpaka sasa tunaongea Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc tulimsaini miaka mitatu na tukamtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 – 2025″
”Mchezaji Yusuph Kagoma haruhusiwi kucheza timu yoyote kutokana na mkabata wake unasoma timu mbili, Hivyo mpaka sasa shauri letu lipo chini ya kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji mpaka sasa hatujasikilizwa”
Huu hapa muamala wa malipo waliofanya Yanga kwenda kwa Fountain Gates
mkataba wa mauziano baina ya Fountain gates,Yanga na Yusuf kagoma