Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema safari za treni za reli ya kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dkt. Biteko ameyasema hayo hii leo Septemba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa mara ya kwanza.

“Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka,” amesema Dkt. Biteko

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha umeme unatosheleza Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha wakati wote na kuongeza kuwa wizara inasimamia ujenzi wa laini nyingine ya kuutoa umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma kwa laini kubwa zaidi na kutoa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kwenda Dodoma baadae Singida, arusha hadi Mwanza.

Huu hapa mkataba wa Yanga na Yusuf Kagoma
Majaliwa: Miradi ya Dola Bilioni 8.65 imesajiliwa ndani ya mwaka