Kampuni ya Mabasi ya Katarama imesitishiwa Leseni ya Usafirishaji kuanzia kesho Septemba 13, 2024 kwa kosa la kuchezea mifumo ya mwenendo iliyowekwa na Mamlaka ya Uthibiti Usafiri Ardhini – LATRA.

Mkurugenzi wa LATRA, Habibu Suluo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wamiliki wa mabasi ya BM Coach, Super Feo, Abood na Katarama.

Amesema, wamiliki wa Kampuni za Bm Coach , Super Feo na Abood wamepewa wiki moja kujirekebisha kutokana na ajali zilizotokea siku za nyuma kwenye mabasi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni kikosi cha usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Nassoro Sisiwayah amesema watafuatilia waliochezea mfumo huo, ili kubaini na kupelekwa Mahakamani wahusika.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi – TABOA, Abdallah Kiongozi ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa mabasi kuzingatia sheria na kanuni za LATRA.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 13, 2024
Dodoma jiji yazamisha jahazi la Zahera